Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web

  Picha na MAKALA za Qur'an 9:
     
NYUMBANI

KUHUSU KURASA

PICHA

NINI KIPYA

ANWANI

VIUNGANISHI CHAGUO

MAKALA NA PICHA 1

MAKALA NA PICHA 2

MAKALA NA PICHA 3

MAKALA NA PICHA 4

MAKALA NA PICHA 5

MAKALA NA PICHA 6

MAKALA NA PICHA 7

MAKALA NA PICHA 8

MAKALA NA PICHA 9

MAKALA NA PICHA 10

 
MAUTI, MAUTI, MAUTI:

Popote mlipo Mauti yatakufikieni, hata mkiwa katika ngome madhubuti.{Qur'an 4:78}

"Kukimbia hakutakufaeni kama mkimbia mauti au kuwa katika vita, na kwa hivyo {hata mkikimbia}hamtaishi ila kidogo {kisha mara mtakufa}" {33:16}

                                        "Kila nafsi itaonja Mauti.Na bila shaka mtapewa ujira wenu kamili siku ya Kiama. Na aliyewekwa mbali na Moto na akaingizwa Peponi basi amefuzu. Maisha ya dunia si kitu ila ni starehe idanganyayo"{3:185}

                                            "Na maisha ya Dunia si kitu ila ni mchezo tu na upuuzi. Na bila shaka nyumba ya Akhera ni Bora zaidi. Basi hamtii akilini?"{6:32}

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA NA MWENYE KUREHEMU. NA HAPANA HILA WALA NGUVU ILA KUTOKA KWA MWENYEZI ALIE JUU KABISA NA MTUKUFU:

 

Assalaam Aleykum.

Na inakingwa shari ya Hasidi kwa anaehusudiwa kwa sababu  zifuatazo; pamoja na Kijicho na Uchawi.

 

Kwanza:

KUJILINDA KWA MWENYEZI MUNGU DHIDI YA SHARI YAKE:

Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwenye kumsikia mwenye kujilinda kwake na ni mjuzi wa kile anachojilinda nacho. 鈥溾€︹€︹€?.jikinge kwa Mwenyezi Mungu kwa hakika yeye ni mwenye kusikia mwenye kuona鈥漿Ghaafir aya ya 56}

 

Pili:

UCHA MUNGU:

Na kumuhifadhi Allah kwa kutekeleza amri zake na kuacha makatazo yake, mtu anaemcha Allah basi Allah nae hutawalia kumhifadhi wala hatamuwakilisha mwingine yeyote 鈥淣a kama mkisubiri na mkamcha Mungu hila zao hazitakudhuruni kitu鈥漿Imran aya ya 120}

 

Tatu:

KUMSUBIRI ADUI WAKO:

Na usimpige vita wala usimseme kwa ubaya, wala usiisemeze nafsi yako kutaka kumuudhi abadani, hutokuwa mwenye kunusuriwa kwa yule hasidi wako na adui wako kwa kitu kuliko kumsubiri na kumtegemea Allah {s.w}. Wala usiuone muda mrefu wa kunusuriwa wala uovu wa adui wako

Kwa hakika kila unapofanyiwa ubaya, ubaya wake yule anayefanya huo ubaya unakuwa ni jeshi na nguvu kwa yule anayefanyiwa ubaya huo na anayehusudiwa. Unampiga vita ubaya wake mwenyewe haliya kuwa yeye hatambui. Uovu wake ni mshare anaopigia nafsi yake mwenyewe. Na laiti kama mtu anayefanyiwa ubaya atayaona haya basi angefurahi kufanyiwa ubaya, lakini kwa udhaifu wa kutambua kwake haoni ila ule ubaya anaofanyiwa na vingine havioni  鈥淣a ajilipizae kisadi sawa na dhara aliyotiwa, kisha  akadhurumiwa tena bila shaka Allah [s.w] atamnusuru鈥漿Hajj aya ya 60}

Na hakuna dhambi ambayo adhabu yake huja haraka zaidi kuliko kufanya ubaya na kukata udugu.

 

Nne:

KUMTEGEMEA MWENYEZI MUNGU:

Na anayemtegemea Allah basi yeye atamtosha. Na kumtegemea Allah ni sababu kubwa kabisa ambayo mja anaweza kujikinga dhidi ya yale asiyoyaweza miongoni mwa maudhi ya viumbe, dhuruma na uadui wao. Kwa hakika Allah anamtosha yaani atamtoshereza.

Na yule ambaye Allah anamtoshereza na anamkinga, adui atakuwa hana tama ya kumpata wala hatodhurika ila kwa madhara ambayo ni ya lazima kama vile joto, baridi, njaa na kiu. Ama kudhuru kwa kufikia anavyotaka yule mwenye kumwombea mwenzie dhara jambo hilo halitotokea abadani 鈥淣a anayemtegemea Allah basi yeye humtosha鈥漿Talaq aya ya 3}

KILA IMANI YA  MJA INAVYOKUWA NDIVYO INAVYOKUWA KWA KUMTEGEMEA ALLAH

 

Tano:

KUUSAFISHA MOYO DHIDI YA KUMSHUGHURIKIA NA KUMFIKIRIA:

Hapa unatakiwa ukusudie kumfuta adui yako ndani ya fikra zako kila unapomkumbuka. Wala usimuogope wala usiujaze moyo wako na ni sababu kubwa kabisa inayosaidia kujikinga na shari yake

Iwapo roho yake itamlazimu na kufungamana na [adui yake] na roho ya hasidi muovu ikafungamana nae akiwa macho na akilala haitokani naehali ya kuwa anatamani roho mbili hizo kulazimiana na kushikamana, na kila roho hiyo inapofungamana na nyengine utakosekana utulivu na shari itadumu mpaka aangamie mmoja wapo. Ama iwapo ataiondosha roho yake kwake na akaikinga kumfikiria tu kufungamana nayo na kutokumtia mawazoni mwake. Iwapo atamtia mawazoni mwake afanye haraka sana kuondoa mawazo hayo na kujishughulisha kwa jambo lenye manufaa zaidi na bora zaidi kwake atabaki hasidi muovu anajila mwenyewe, kwani hakika ya husda ni kama moto iwapo hautopata cha kukila utajila wenyewe kwa wenyewe

Na mlango huu una nafuu kubwa ambayo hawaipati ila watu wenye nafsi tukufu na hima kubwa{Ama mwenye chuki anaetaka kulipiza kisasi na kumtambua adui wake hatoyapata haya.

 

Sita:

KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU NA KUMFANYIA IHSANI:

 Weka mapenzi yako, ridhaa yako na kurejea kwake Allah, mawazo yako na matakwa yako yawe yanakwenda katika mwenendo huo pole pole mpaka uyashinde mawazo yako uyatoe na uyaondoshe yote na yabakie mawazo yako na fikra zako na matakwa yako  katika kumpenda Mwenyezi Mungu, na kujikurubisha kwake, kumhangaikia, kumridhisha, kutaka huruma zake na kumkumbuka kama unavyomkumbuka mpendwa wako wadhati. Utakapotekeleza haya itazidi kukuepesha na husda, uovu chuki n.k.

鈥淗akika shetani yeye hana nguvu juu ya wale walioamini na wanaomtegemea Mola wao, nguvu zake ni juu ya wale wanaomfanya rafiki{wakamfuata}na juu ya wale wanaomshirikisha Allah nae.{Nahal aya ya 99-100}

Ni furaha kubwa iliyoje kwa aliyeingia katika himaya hii na akawa ndani ya ngome madhubuti. Ameshaingia katika himaya ambayo mtu aliyejihami nayo atakuwa hana khofu yoyote, wala hatopotea, wala adui hatokuwa na tama ya kumkaribia.

Hiyo ni fadhira ya Mwenyezi Mungu anayompa amtakae, na Mwenyezi Mungu mwenye fadhira kuu.

 

Saba:

KUMTAKASIA TOBA MWENYEZI MUNGU:

鈥淣a misiba inayokupateni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu鈥?

{Shuura aya ya 30} Basi hatotokezea mtu kuja kumuuzi mja ila kwa sababu ya madhambi aliyoyafanya sawa kama anayajua au hayajui. Dhambi ambazo mja hazijui ni nyingi zaidi kuliko zile anazozijua na zilealizozisahau katika alizozifanya ni nyingi zaidi kuliko anazozikumbuka . Na imekuja katika dua mashuhuri 鈥淓we mola wangu hakika mimi ninajilinda kwako nisikushirikishe hali ya kuwa ninajua na ninakuomba msamaha kwa yale nisiyoyajua鈥?/FONT>

hivyo mja madhambi yake ambayo anatakiwa kuyaombea msamaha katika asiyoyajua ni mengi zaidi na zaidi kuliko yale anayoyajua, hivyo hatotokomezwa adui ila kwa dhambi {aliyoifanya} moja wapo ikiwa ni Husda, Uchawi na Kijicho.

Hivyo mja iwapo atafanyiwa uovu au ataudhiwa hatopata kitu chenye manufaa zaidi kwake kuliko kutubu toba ya kweli.

 

Nane:

UKWELI NA IHSANI KWA KADRI INAVYOWEZEKANA:

Kwa hakika jambo hili lina taathira ya ajabu katika kukinga mabalaa kukinga vijicho, Shari ya Hasadi na laiti kama hakuna haya ila majaribio ya umma mbali mbali zilizopita na zilizopo basi ingetosha kuwa ushahidi. Hutoona kijicho, Husda na udhia ukielekezwa kwa mtu anayefanya ihsani na aliye mkweli

Na iwapo kitamsibu kitu katika hivyo basi utaona anapata huruma, msaada na nguvu na mwisho wake utamalizika kwa jambo zuri, mtu mwenye ihsani na mkweli atakuwa katika himaya ya ihsani yake, na ukweli wake utakuwa ni ngome madhubuti na kizuizi kihifadhicho kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa ujumla shukrani ni mlinzi wa neema kwa kila ambaye atakuwa ni sababu ya kuondoka kwake hiyo neema.

Na miongoni mwa sababu kubwa sana za husda ya hasidi na mwenye kijicho, ni kuwa haidhoofishi husda yake wala hakinyamazi kilio chake wala haupoi moyo wake mpaka iondoke neeema kwa yule anayemuhusudu. Hapo ndipo kitaondoka kilio chake na utazimika moto wake

Hivyo hakuna jambo kubwa ambalo mja anaweza kuilinda neema yake hiyo, wala hakuna litakalopelekea kuondoka neema hiyo kuliko kuifanyia maasi kwa Mwenyezi Mungu, na huko ndiko kukufuru neema na ni mlango unaopelekea kumkufuru yule mwenye kuneemesha.

Kwa hiyo mtu wa ihsani aliye mkweli anatumia majeshi na askari wanaopigana kwa ajili yake hali ya kuwa yeye amelala kitandani pake. Na asiyekuwa na jeshi wala askari na akawa na maadui, basi maadui zake watamshinda hata kama muda wake wa kushindwa utachelewa.Mwenyezi Mungu ndiye wa kutegemewa.

 

Tisa:

KUUZIMA MOTO WA HASIDI, MAOVU NA MWENYE MAUDHI KWA KUMFANYIA IHSANI:

Na hii ni miongoni mwa sababu ngumu kabisa kwa nafsi na ni yenye mashaka zaidi wala hawawafikishiwi kuifikia ila watu wenye hadhi kubwa kwa Mwenyezi Mungu {wacha mungu} nayoni kuuzima moto wa Hasadi, Muovu na Mwenye Maudhi kwa kumfanyia Ihsani kila anapokuzidishia maudhi, shari uovu na husda wewe umzidishie ihsani, umnasihi na kumuhurumia. Na si zani kuwa kama utasadiki kuwa jambo hili litaweza kuwa sembuse wewe kulifanya. Hebu msikilize Allah{s.w}

鈥淣a wala hayawi sawa mazuri na mabaya. Ondosha {ubaya unaofanyiwa kwa wema} tahamaki yule ambaye baina yako na baina yake kuna uadui atakuwa  kama ni jamaa {yako} mwenye kukufia uchungu. Lakini jambo hili hawatapewa ila wale wenye kusubiri, wala hawatapewa ila wale wenye hadhi kubwa {kwa Mwenyezi Mungu} Na kama shetani atakushawishi kwa tashwiwishi {zake ili ugombane na hao wanaokufanyia ubaya} wewe jikinge kwa Mwenyezi Mungu kwa hakika yeye ni mwenye kusikia, mwenye kujua鈥?{Fuswilat aya ya 34-36}

鈥淏asi hao watapewa ujira wao mara mbili kwa kusubiri kwao na kuondoa ubaya kwa wema na kutoa katika yale tuliyowapa鈥漿Qasas aya ya 54}

Mtu {s.a.w} alipigwa sana na wapinzani wake {watu} mpaka wakamto damu akawa anajipangusa damu huku anasema  鈥淓we Allah wasamehe watu wangu kwa hakika wao hawatambui鈥?/FONT>

Kwa hiyo unatakiwa utekeleze haya katika ihsani

  1. Kuwasamehe
  2. Kuwaombea msamaha
  3. Kuwatafutia udhuru kuwa hawatambui
  4. Kuwahurumia kwa kuwafungamanisha  nae kwa kusema 鈥榳asamehe鈥?/FONT>

Jamaa mmoja alikwenda kuwashitaki ndugu zake kwa Mtume {s.a.w.} kuwa awafanyia ihsani lakini wao humfanyia ubaya. Mtume akamwambia 鈥渦taendelea kuwa pamoja nawe msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu muda wote utakaodumu katika jambo hilo.

 

Kumi:

KUMPWEKESHA ALLAH PEKE YAKE:

Na sababu hii inakusanya yote niliyotangulia kuyaeleza na ndio mzunguko wa sababu hizo zote. Nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu peke yake na kusafiri kimawazo katika sababu mpaka kwa mwenye kuisababisha ambaye ni mwenye nguvu na mwenye hekma, na kufahamu kuwa ala zote ni mfano wa yanayofanywa na upepo ambao nao umo katika mikono ya anaeutuma, alieumba na alieanzisha. Wala hauwezi kudhuru wala kunufaisha ila kwa idhini yake. Nae ndie anaemneemesha mja wake kwao nae pekee ndie awezae kumuondoshea madhara yake hakuna mwengine asiyekuwa yeye.

鈥淣a kama  Mwenyezi Mungu akikugusisha dhara, basi hakuna yeyote awezae kuiondoa isipokuwa yeye, na kama akikutakia kheri basi hakuna awezae kurudisha fadhira zake鈥漿Yunus aya ya 107}

Amesema Mtume {s.a.w} Na tambua kuwa lau kama umma utakusanyika ili wakunufaishe kwa kitu, hawatoweza kukunufaisha ila kwa kitu ambacho amekwisha kukuandikia Mwenyezi Mungu ukipate na lau kama watakusanyika kukudhuru kwa kitu hawatoweza kukudhuru ila kwa kitu ambacho amekuandikia Mwenyezi Mungu kikufike.

Iwapo mja atampwekesha Mwenyezi Mungu peke yake basi itatoka katika moyo wake khofu isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu na adui wake atakuwa ni mwepesi mno kwake kwa vile hatomuogopa bali anamuopa Menyezi Mungu pekee hivyo atasalimika nae, na yatatoka moyoni mwake mawazo yake na kumshughurikia na atabaki na mapenzi ya Mwenyezi Mungu tu, khofu yake, kurejea kwake, kumtegemea yeye na kumshughurikia yeye bila ya kumuingiza mwengine. Na ataona kuwa kufikiria habari za adui wake.kumuogopa na kumshughurikia ni katika upungufu wa tawhiid yake, na lau kuwa angempwekesha Allah peke yake basi angekuwa Allah ndiyo shughuri ya kumshughulikia. Allah atasimamia  kumuhifadhi na atamlinda kwani Mwenyezi Mungu huwakinga wale walioamini iwapo ni muumini basi Mwenyezi Mungu lazima atamkinga, na imani yake inatosha kuwa sababu ya kukingwa na Allah. Na iwapo imani yake imekamilika basi hifadhi ya Allah kwake itaimalika zaidi, na iwapo atachanganya nae basi atachanganyiwa, na iwapo ni mar kwa mara na Allah atamfanyia mara kwa mara huyo mja

Atakaye mwende Allah Mzima mzima nae Allah atamwendea  jumla jumla, atakaye mpuuza Allah yeye mzima Allah naye atampuuza kwa jumla, na atakayefanya kwa muda na Allah nae atafanya muda na muda.

Hivyo Tawhiid ni ngome ya Allah iliyo kubwa kabisa atakayeingia atakuwa ni miongoni mwa waliosalimika.  Wamesema baadhi ya watu wema waliopita kuwa [Anayemuogopa Allah ataogopwa na kila kitu, na asiye muogopa Allah atamuogopesha kila kitu]

 

Hizi ni sababu kumi ambazo hukingwa shari ya Hasidi, mwenye Kijicho na Mchawi, na hakuna kinga bora zaidi ya kuliko kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, kumtegemea na kuwa na thika {uhakika} nae, na asimuogope yeyote pamoja nae, bali khofu yake inakuwa kwa Allah peke yak, wala hataraji chochote kwa asiyekuwa yeye mmoja tu,moyo wake haufungamani na yeyote asiyekuwa yeye, wala hataki msaada kwa asiye kuwa Allah. Na wakati moyo wake unapofungamana na mwengine, na ukamtarajia na kumuogopa basi hufanywa mtumwa wake na hudhalilishwa kwa upande wake. Na anayeogopa kitu hicho juu yake, na anayetaraji kitu kwa asiyekuwa Allah atadhalilishwa kwacho na atanyimwa kheri yake na huu ndiyo mwenendo wa Allah kwa viumbe vyake na wala hutokuta katika mwenendo wa Mwenyezi Mungu mabadiliko. 

 

 

                       

 

 

Qur'an:
Maajabu ya nzi
Maajabu ya Nyuki:

Vitabu vya Mwenyezi Mungu:
Qur'an:
Itikadi Sahihi:
 
   
 

Uislamu ni Ngozi ya Mwili sio Vazi la Kuvua!!!